HabariMilele FmSwahili

Majengo katika ardhi ya Shirika la reli yabomolewa Kwa Njenga, Nairobi

Wakazi katika kijiji cha Kwa Njenga eneo la Imara Daima hapa jijini Nairobi wanakadiria hasara kufuatia ubomozi wa nyumba zao. Ubomozi huo unaarifiwa kutekelezwa kutokana na makaazi hayo kujengwa katika eneo la reli. Wakazi hao wameshutumu ubomozi huo uliotekelezwa na maafisa wa mashirika ya reli wakishirikiana na wa kampuni ya umeme Kenya Power na polisi. Wanasema licha ya kupokea notisi ya kuondoka eneo hilo hawakufahamishwa kuhusu ubomozi.

Show More

Related Articles