HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wabunge wamekiri kutumiwa picha za aibu na mwanamke asiyetambulika

Kulikuwa na msisimko bungeni baaada ya wabunge kudai kuwa kuna mwanamke anayewatumia picha za uchi wake kwenye simu zao za mkono.
Hii ni kando na wahuni kuandikisha laini zao za simu kwa kutumia majina ya wabunge, na kutumia laini hizo kutapeli wabunge wengine na wananchi kwa jumla.
Mwakilishi wa wanawake kutoka kaunti ya Murang’a Sabina Chege ndiye aliyezua hoja hiyo, huku spika wa bunge Justin Muturi akitaka maafisa wasimamizi wa masuala ya usalama nchini kufika mbele ya kamati ya bunge kuhusu usalama katika muda wa siku saba.

Show More

Related Articles