HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Rais amteua Noordin Haji kama Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma

Rais Uhuru Kenyatta sasa amemteua Noordin Mohamed Haji kama mkurugenzi wa mashtaka ya umma, kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na waziri wa mazingira Keriako Tobiko.
Haji ambaye ni afisa mkuu katika idara ya ujasusi -NIS, alikuwa miongoni mwa watahiniwa 10 waliofika mbele ya jopo la uteuzi wiki jana, na akawa mmoja kati ya watatu waliochaguliwa na majina yao kuwasilishwa mbele ya rais Kenyatta.
Noordin Haji sasa anasubiri kuidhinishwa na bunge kabla ya kuapishwa, kama anavyotuarifu Kiama Kariuki.

Show More

Related Articles