HabariMilele FmSwahili

Mbunge wa Mavoko atimuliwa bungeni baada ya kukatalia kwenye kiti rasmi cha kiongozi wa wachache

Mbunge wa Mavoko Patrick Makau ametimuliwa bungeni alasiri ya leo baada ya kukatalia kwenye kiti rasmi cha kiongozi wa wachche John Mbadi. Juhudi za kumsihi mbunge huyo kumpa nafasi mbadi kukatili kiti chake zilikosa kuzaa matunda hali iliyommlazimu spika Justin Muturui kuagiza aondolewe kwa nguvu na kuagizwa kutohudhuria vikao vya leo Alasiri. Aidha mwakilishi akina mama kaunti ya Vihiga Beatrice Adagala naye aliagizwa kuondoka kaitka kiti kilichotengewa kiranja wa wachache Junet Mohammed. Yadaiwa walikuwa wamechukau nafasi hizo kulalamikia mkutano ulioandaliwa baina ya Raila Odinga na rais Uhuru Kenyatta

Show More

Related Articles