HabariPilipili FmPilipili FM News

Wabunge Wa ODM Waunga Mkono Azimio La Raila Kuunganisha Wakenya.

Viongozi wa chama cha ODM wamekutana na kukubaliana kuunga mkono azimio la Raila Odinga  kushirikiana na serikali katika kuunganisha taifa la kenya.

Akiongea kwa niaba ya viongozi wa chama cha ODM mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed amemtaka Raila Odinga kutumia  ushirikiano  wake na raisi  Uhuru Kenyatta kutafuta haki ya wote walioathirika na machafuko ya baada ya uchaguzi.Nao viongozi wa chama cha Wiper wakiongozwa na David Musila wanasema viongozi hao wawili wameonyesha mfano mzuri kwa taifa hili, na kwamba hatua yao itasaidia kurejesha uthabiti wa taifa hili.

Show More

Related Articles