HabariPilipili FmPilipili FM News

Noordin Mohammed Ateuliwa Na Rail Kuwa Mkurugenzi Wa Mashtaka Ya Umma.

Rais Uhuru Kenyatta amewasilisha jina la Noordin Mohammed Haji kwa bunge kupigwa msasa ili kuhudumu kama mkurugenzi wa mashtaka ya umma.

Rais amependekeza jina la Haji kutoka kwa orodha ya wakenya watatu waliopendekezwa na jopo lililowahoji wakenya 10 waliotuma maombi ya kuteuliwa kwenye wadhfa huo.

Pia amewasilisha jina la jaji Paul Kihara Kariuki bungeni kupigwa msasa ili kuhudu kama mkuu wa sheria.

Pia amewateua mhandisi John Musonik kuwa katibu mkuu wa utawala CAS katika wizara ya petroli na madini, Hassan Noor katika wizara ya michezo na Mohamed Ibrahim Elmi wa mazingira.

Show More

Related Articles