HabariMilele FmSwahili

Wabunge wa ODM waidhinisha mazungumzo baina ya kinara wao Raila na Rais Uhuru

Wabunge wa ODM wameidhinisha mazungumzo baina ya kinara wao Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta. Katika taarifa ya pamoja baada ya mkao wao,kiranja wa wachache bungeni Junet Mohammed amesema wameridhishwa na mazungumzo baina ya rais Kenyatta na Raila wakiyataja kama yatakayoliunganisha taifa hili. Wamemtaka Raila kuwapuuza wanaomshtumu kwa kukubaliana kufanya kazi na rais Kenyatta wakiwataka kama wabinafis wasiojali maslahi ya wakenya.

 

 

Show More

Related Articles