HabariPilipili FmPilipili FM News

NACADA Yasaka Pombe Haramu Kaunti Ya Kilifi.

Shirika la kupambana na dawa za Kulevya nchini NACADA kwa ushirikiano na asasi za usalama, linaendeleza msako dhidi ya pombe haramu mjini  Malindi  Kaunti ya Kilifi, kwa lengo la kumaliza pombe hiyo humu nchini.

Afisa mkuu wa NACADA eneo la pwani George Karisa anasema tayari watu wawili wametiwa mbaroni kufuatia oparesheni hiyo, kwa kujaribu kuzuia maafisa husika kuendesha msako wao eneo hilo.

Kamishna wa kaunti ya Kilifi Magu Mutindika ameowaonya wenye baa wanaokiuka sheria za vileo kwamba baa zao zihtafungwa, na wao kuchukuliwa hatua kali kisheria.

 

Show More

Related Articles