HabariPilipili FmPilipili FM News

Sehemu Ya Barabara Ya Nairobi-Mombasa Yafungwa Kutokana Na Ajali Ilyotokea Asubuhi.

Sehemu ya barabara kuu ya Mombasa- Nairobi imefungwa kwa mda kufuatia ajali iliyohusisha Lori la kusafirisha gesi na lengine lililokuwa limebeba kontena usiku wa kuamkia leo.

Ajali hiyo iliyotokea eneo la Chyulu imesababisha msongamano mkubwa wa magari, hali ambayo inahofiwa kukwamisha kabisa shughuli za uchukuzi, katika barabara ya mombasa nairobi.

Maafisa wa polisi walilazimika kuzuia magari kutumia sehemu hiyo ya barabara, baada ya Lori la kusafirisha gesi kushika moto.

Tungali tunafuatilia taarifa hii na tutaweza kukupasha kwa kina zaidi katika awamu nyingine ya taarihfa zetu.

Show More

Related Articles