HabariMilele FmSwahili

António Guterres apongeza Rais Uhuru na Raila kwa kufikia makubaliano ya kushirikiana

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewapongeza rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kufikia makubaliano ya kushirikiana kuhimiza Umoja wa taifa. Msemaji wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Stephane Dujarric amesema Antonio Guterres ameridhishwa na hatua ya wawili hao kukubaliana kuwaunganisha wakenya. Guterres pia ameahidi kushirikiana na serikali katika kuimarisha amani, utulivu na maendeleo.

Show More

Related Articles