HabariMilele FmSwahili

Jopo lapendekeza Hajji,Kambuni na Nyakundi kuwania nafasi ya DPP

Jopo lililoendesha mahojiano ya kumteu mkurugenzi wa mashtaka ya umma sasa limependekeza majina ya Noordin Hajji, Lucy Kambuni na Jacob Nyakundi kuwania nafasi ya mkurugenzi mkuu wa mashitaka ya umma. Jopo hilo linaloongozwa na Elizabeth Muli limeafikia orodha ya watatu hao kutoka watu kumi waliopigwa msasa wiki jana. Rais Kenyatta anatarajiwa kuteua mmoja wao na kuwasilisha jina lake bungeni kwa ukaguzi zaidi na iwapo ataidhinishwa ataapishwa kujaza nafasi ilioachwa na Keriako Tobiko ambaye sasa ni waziri wa mazingira.

Show More

Related Articles