HabariMilele FmSwahili

Mtu 1 afariki baada ya lori mbili kugongana eneo la Chyulu Hills katika bara bara ya Mombasa Nairobi

Mtu mmoja amefariki na wengine watatu kujeruhiwa baada ya lori mbili  kugongana katika eneo la Chyulu Hills kwenye bara bara ya Mombasa Nairobi. ajali hiyo ilihusisha trela la kusafirisha mizigo na lori la kusafirissha gesi. aidha imepelekea bara bara hiyo kufungwa huku kamanda wa polisi eneo la taitataveta fred ochieng akiwashauri madereva kuepuka eneo hilo juhudi zikiendelea kuyaondoa malori hayo yaliyofunga bara bara. magari yote yanayoelekea nairobi kutoka mombasa pia yameelekezwa kutumia barabara ya Voi Taveta Oloitoktok, huku yale ya kutoka Nairobi yakitakiwa kutumia barabara ya Loitoktok,Taveta Voi.

Show More

Related Articles