BiasharaMilele FmSwahili

Kampuni ya Telkom yazindua huduma ya kutuma na kupokea pesa T-Kash

Kampuni ya mawasiliano ya Telkom imezindua aina mpya huduma za kutuma na kupokea pesa kwa jina ya T kash. Tayari kuna zaidi ya maajenti wa huduma 20,000 katika miji tofauti nchini wanaotoa huduma hizo. Akiongea wakati wa uzinduzi huo afisa mkuu mtendaji Aldo Mareuse anasema huduma hiyo mpya itakuwa bora zaidi na yenye kuwafaa wateja wake. Mareuse ameelezea matumaini yake akisema Kuwa tayari idadi ya wateja wa Telkom imeongezeka kwa milioni moja miezi 9 baada ya kampuni ya helios kuchukua umiliki kwenye kampuni hiyo.

Kwa upande wake waziri wa habari na teknolojia Joe Mucheru anasema kenya imepata sifa kimataifa kutokana na huduma hizo za kutuma na kupokea fedha.

Show More

Related Articles