HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta atetea utendakazi wa waziri wa elimu balozi Amina Mohammed

Rais Uhuru Kenyatta ametetea utendakazi wa waziri wa elimu Amina Mohammed akisema ana uwezo kuleta mageuzi hitajika kwenye wizara hiyo. Akizungumza alipowakabidhi wanafunzi 100 tuzo zinazotambua mchango wao kwa jamii, rais amesema kinyume na madai kwamba waziri Fred Matiang’ alielewa sana yalio kwenye wizara hiyo,waziri Amina anaelewa zaidi yaliomo wizarani na atachapa kazi yake inavyostahili. Ametaka apewe uungwaji mkono hitajika na wadau wote kuhakikisha sekta ya elimu inaendelea kuimarika.

Show More

Related Articles