HabariPilipili FmPilipili FM News

Bangi Yenye Thamani Ya Laki Moja Unusu Yanaswa Kwale

Maafisa wa polisi kaunti ya Kwale wamenasa  bangi  yenye thamani ya shilingi  laki moja unusu eneo la mbuguni , matuga mapema hii leo.

Akithibitisha tukio hilo Naibu kamishna wa Matuga Benson Maisori amesema oparesheni hiyo iliendeshwa mwendo wa tisa unusu, bada ya polisi  kupashwa habari na wananchi kuhusu jamaa aliyepatikana akiwa amebeba   mizigo katika hali tatanishi.

Maisori amesema bangi hiyo ilitolewa kaunti ya mombasa na ilikua ikisafirishwa maeneo ya Diani na Ukunda.

Amepongeza wananchi kwa ushirikiano mzuri na mafisa wa polisi huku uchunguzi ukianzishwa kumsaka mshukiwa ambaye alitoweka baada ya kugundulika

Show More

Related Articles