HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Madaktari wanagenzi 700 wangali kurejea kazini licha ya agizo

 

Shughuli za matibabu bado zimeathiriwa katika hospitali kuu ya Kenyatta huku ,madaktari wanagenzi wapatao mia saba waliogoma wakikosa kurejea kazini licha ya kuagizwa na mwenyekiti wa bodi inayosimamia madaktari nchini KMPDB kurejea kazini.

Aidha katibu mkuu wa muungano wa madaktari-KMPDU Ouma Oluga, amesema kuwa muungano huo unaunga mkono agizo la wanafunzi hao kurejea kazini ila tu ipo haja bodi ya KMPDB kufuata njia mwafaka ya kuwarejesha kazini wanafunzi hao.

Show More

Related Articles