HabariMilele FmSwahili

Washukiwa 23 wa sakata ya ubadhirifu wa milioni 47 za NYS waondolewa mashtaka

Washukiwa 23 wa sakata ya ubadhirifu wa shilingi milioni 47 katika shirika la NYS wameondolewa mashtaka. Hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Kenneth Bidali anasema upande wa mashtaka umekosa kuwasilisha ushahidi tosha kudhibitisha 23 walihusika katika wizi wa fedha hizo. Kadhalika Bidali ameongeza kwamba upande wa mashtaka umeshindwa kudhibitisha ifaavyo uzito wa kesi hiyo. Mwaka 2016, washukiwa wengine 11 waliohusishwa na sakata hiyo kesi dhidi yao pia ilitupiliwa mbali kwa ukosefu wa ushahidi. Walioponea leo ni pamoja na aliyekuwa katibu Peter Mangiti na aliyekuwa mkuu wa NYS Nelson Githinji

Show More

Related Articles