HabariPilipili FmPilipili FM News

Uhuru Na Raila Wakubaliana Kufanya Kazi Pamoja

Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa muungano pinzani hapa nchini wamefanya  kikao cha faragha katika jumba la Harambee jijini Nairobi.

Akihutubia taifa baada ya kikao hicho Rais Uhuru Kenyatta amesema Kenya ni kubwa kuliko mtu yeyote hivyo ipo haja ya kushirikiana na kila mtu  ili taifa iweze kupiga hatua kimaendeleo.

Kwa pande wake  Raila Odinga amesema kuwa  ipo haja ya Wakenya kuhakikisha kwamba wanaishi kwa utangamano kwa faida ya taifa na wala sio kwa msingi wa tabaka hili au lile kujiona bora

Viongozi hao wawili wamekubaliana kuweka tofauti zao kando na kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya wakenya.

Show More

Related Articles