HabariMilele FmSwahili

Rais Uhuru na Raila waamua kuweka kando tofauti zao za kisiasa

Rais Uhuru Kenyatta na mpinzani wake Raila Odinga wameamua kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kuwahudumia wakenya. Wakizungumza baada ya mkutano wao wa saa moja katika jumba la Harambee, Rais Kenyatta anasema wamekutana na Raila na kuamua kwamba wakati wa siasa na kwamba ni lazima taifa lisonge mbele. Rais,anasema kwa muda mrefu siasa imeligawa taifa hili kwa misingi ya kikabila na hata kuwafanya wakenya kupoteza maisha yao.

Kwa upande wake Raila anasema wakati umefika wakenya kuweka kando tofauti zao na kusonga mbele.

Raila anasema iwapo taifa litasalia kugawanyika basi hiyo ni hatari kwa umoja wa baadaye wa taifa hili.

Mwafaka wao ukijiri saa chache tu kabla ya katibu wa masuala ya kigeni wa marekani Rex Tillerson kuwasili nchini kwa mazungumzo na viongozi hao wawili.

Show More

Related Articles