HabariPilipili FmPilipili FM News

Shirika La KWS Lalaumiwa Kushindwa Kudhibiti Wanyama Pori Taita.

Aliyekuwa mbunge wa Wundanyi Thomas Mwadeghu amelinyoshea kidole cha lawama shirika la kuhifadhi wanyama pori KWS kwa kushindwa kudhibiti wanyamapori kuingia katika makaazi ya wananchi.

Mwadeghu amesema ni jambo la kusikitisha kuona kuwa shirika hilo linaweka ua wa umeme kuizunguka mbuga ya Tsavo bila kufuata mipaka sahihi bali inasongezwa kwa ardhi za wakaazi.

Aidha amewataka viongozi wa kaunti hiyo kushirikiana na viongozi katika serikali ya kitaifa hususan waziri wa utalii na katibu wa mazingira kupanga mikakati jinsi ya kuziua mwingiliano wa wanyama na binadamu.

 

Show More

Related Articles