BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Msanii Dogo Richie Adai Kurogwa Baada Ya Kuimba Mziki Majanga.

Baada ya kuimba mziki majanga na kuwataja baadhi ya wasanii kutoka pwani sasa kibao kimegeuka na majanga yameanza kumrudia mwenyewe msanii Dogo Richie  na sasa anapata shida akiingia studio sauti yakwama.

Akihojiwa ndani ya Pilipili Fm kwenye kipindi cha Mwake Mwake Live na Chigz Ngala masanii Dogo Richie aliweka wazi matatizo yake akidai kurogwa na sasa sauti yake imekua ikipotea kila akiingia studio kujaribu kurekodi ngoma.

“Yeah sasa hivi hali yangu kwa kweli sio shwari na naamini nimerogwa na mmoja ya wasanii niliowataja kwenye ngoma ya mziki majanga coz nikiingia studio sauti yakwama kabisa “. Amesema msanii huyo.

Wasanii waliotajwa kwenye ngoma hio ni pamoja na Susumila,Nyota Ndogo,Chikuzee Ally B, Bawazir,Bizzy K, Kaa La Moto, Fat S na wengine na mpaka saa hii haijabainika nani kati ya hawa amemwendea kinyume Dogo Richie na kupoteza sautu yake.

Msanii hata hivyo amepinga madai ya baadhi ya wapinzani wake kuwa amebuma kimziki na anatafuta KIKI zakufufuka tena akisema hajaishiwa na hali aliyonayo imemsibu kwa kipindi cha miezi mitatu sasa.

But amesema ataelekea kwa Mhubiri wa kanisa kunusuru hali yake.

Show More

Related Articles