HabariPilipili FmPilipili FM News

Vitabu Vya Mtaala Mpya Kufanyiwa Marekebisho

Wizara ya elimu nchini imehakikisha kuwa vitabu vya masomo vilivyosambazwa katika shule za umma ni za hadhi ya juu ikisema makosa madogo yaliyobainika yanarekebishwa.

Katibu katika wizara ya elimu Belio Kipsang amesema mradi huo wa vitabu uliogharimu shilingi bilioni 7.5 uko imara na kuwa taasisi ya maendeleo ya mtaala nchini inashughulikia makosa hayo.

Haya yanajiri baada ya chama cha walimu kutaka vitabu hivyo viondolewe shuleni kufuatia makosa yalipatikana haswa katika masomo ya lugha na hisabati.

Show More

Related Articles