HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Bodi ya KNH imewarejesha kazi wahudumu waliokuwa wamesimamishwa

Bodi ya hospitali kuu ya Kenyatta imewarejesha kazi wahudumu wa afya waliopewa likizo ya lazima, kufuatia sakata ya masihara ya upasuaji katika hospitali kuu ya Kenyatta.

Haya yanajiri baada ya bodi hiyo kushiriki kikao na waziri wa afya Sicily Kariuki pamoja na bodi inayosimamia madaktari nchini -KMPDB chini ya mwenyekiti George Magoha, pamoja na baraza la wauguzi nchini kuafikia uamuzi wa bodi ya KMPDB kuendeleza shughuli za uchunguzi wa kisa hicho. Hata hivyo, hatima ya afisa mkuu mtendaji Lily Koros bado haijabainika.

Show More

Related Articles