HabariMilele FmSwahili

Waziri Monica Juma apuuza madai serikali imewatelekeza raia wake katika magereza ya kigeni

Waziri wa masuala ya kigeni Monica Juma amepuuza madai serikali imewatelekeza raia wake wanaozuiliwa katika magereza ya kigeni. Monica anasema mbali na wakenya 1,300 wanaotumikia vifungo katika mataifa ya nje,Kenya pia imewafunga zaidi ya raia wa kigeni 2,000 wote hao wakikabiliwa na makosa tofauti. Anasema wakenya 47 wamefungwa Uganda, 79 Tanzania na 15 Ethiopia.

Kadhalikaanasema Kenya inalenga kupata nafasi ya uanachama katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa.

Vile vile amewataka wakenya wote walio nje ya taifa kujisajili katika balozi za Kenya kuhakikisha wanatambuliwa na kupewa msaada kunapotekea dharura.

Show More

Related Articles