HabariPilipili FmPilipili FM News

Vijana Wa Kwale Watoa Hisia Kinzano Kuhusu Kupigwa Marufuku Kwa Miraa.

Hisia mseto zimeibuka  miongoni  mwa  vijana  wa  kaunti  ya Kwale baada ya  bunge la kaunti hiyo kupitisha  hoja  inayolenga kupiga marufuku utumizi wa mogokaa na miraa katika kaunti hiyo.

Kwenye mahojiano kijana Pepe Haji Nassir  amesema badala ya bunge la kaunti  kupiga marufuku utumizi wa  mogokaa na miraa  miongoni mwa vijana  wangetafuta mwafaka  wa ajira kwa vijana  akisema kuwa ukosefu wa kazi ndio chanzo kikuu cha utumizi wa mogokaa.

Baadhi ya vijana wameonekana na mtazamo tofauti wakisema wanaunga mkono bunge la Kwale mia kwa mia wakisema utumizi wa mogokaa na miraa umeathiri pakubwa maendeleo ya vijana Kwale.

 

Show More

Related Articles