HabariPilipili FmPilipili FM News

Aliyechapisha Taarifa Ya Kumchafulia Jina Gavana Samboja Atafutwa.

Polisi kaunti ya Taita Taveta wameanzisha uchunguzi dhidi ya mwanamume mmoja anayedaiwa kuchapisha habari za kumharibia sifa gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja.

Inasemekana mwanamume huyo aliyetiwa mbaroni jana anaendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi Cha Wundanyi huku akiwasaidia maafisa wa polisi na habari muhimu dhidi ya madai hayo.

Akithibitisha haya Kamanda wa polisi kaunti ya Taita Taveta Fredrick Ochieng’ amedokeza kuwa mshukiwa atafikishwa Mahakamani pindi uchunguzi wa polisi utakapokamilika.

Show More

Related Articles