HabariMilele FmSwahili

Siku ya figo yaadhimishwa kote ulimwenguni leo

Huku siku ya figo ikiadhimishwa kote ulimwenguni leo imenainika kuwa visa vya tatizo la figo miongoni mwa watoto vinazidi kuripotiwa nchini. Kulingana na madaktari katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Eldoret asilimia 6 ya wagonjwa wanaotibiwa maradhi hayo katika hospitali hiyo ni watoto. Madaktari hao wanasema ukosefu wa kinga ni mojawapo ya sababu za ongezeko hilo. Aidha wanasema wanawake nchini wanaokumbwa na matatizo ya figo hupata ugumu kupokea figo mpya kutokana na dhana potofu katika jamii.

Show More

Related Articles