HabariMilele FmSwahili

Amnesty International yataka polisi aliyemuua kiongozi wa wanafunzi wa chuo cha Meru kuchukuliwa hatua

Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International limetoa wito kwa polisi kuchunguza na kumchukulia hatua za kisheria polisi anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi kiongozi wa wanafunzi katika chuo kikuu cha Meru Evans Njoroge. Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo humu nchini Irungu Irũngũ Houghton ameitaka idara ya polisi kuhakisha uchunguzi huru na haki kutendeka kufuatia mauaji hayo. Aidha anaitaka mamlaka ya kuangazia utendakazi wa polisi ipoa kuanzisha uchunguzi wake. Irungu pia amepongeza hatua ya waziri wa elimu balozi  Amina Mohamed kuomba radhi na kumtuma likizo la mapema naibu chansela wa chuo cha Meru Japheth Magambo. Mwanafunzi huyo aliyeuwawa Jumanne wiki iliyopita atazikwa leo nyumbani kwao eneo la Longonot

Show More

Related Articles