HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

IEBC yakashifu NASA kwa kudai haitaaminika katika uratibu wa mipaka

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka, IEBC, Wafula Chebukati amekashifu hatua ya muungano wa NASA ya kudai kuwa tume yake haipo tayari na haitaaminika kwenye zoezi la kuratibu upya mipaka ya maeneo bunge na wadi kama inavyohitajika kikatiba.

Madai ya NASA yanayotokana na kutoridhika kwake na mkondo wa mambo baada ya kura ya marudio ya urais Oktoba mwaka jana yanawadia wakati tume ya IEBC imo mbioni kuwahamasisha wakenya kuhusiana na zoezi hilo kuu linalofaa kuanza hivi karibuni.

Show More

Related Articles