HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Waititu atia saini sheria ya kudhibiti matumizi ya pombe

 

Vita dhidi ya pombe haramu katika kaunti ya Kiambu vimeshika kasi ambapo gavana ferdinand waititu ametia sahihi sheria ya kudhibiti matumizi ya vileo katika kaunti hiyo ikiwa ni miongoni mwa kaunti 25 zilizoathirika na matumizi ya pombe haramu.

Waititu amefutilia mbali leseni za uuzaji pombe na kuwataka wafanyibiashara hiyo kujisajili upya ili kukabiliana na wauzaji pombe haramu. Hayo yakijiri aliyekuwa mwenyekiti wa shirika la kupambana na dawa za kulevya, NACADA ,John Mututho, ameteuliwa kama mshirikishi maalum atakayeongoza operesheni hiyo inayotishia kulemaza kaunti ya kiambu.

Show More

Related Articles