HabariMilele FmSwahili

Watu 15 walazwa hospitalini kutokana na Homa ya Nguruwe Laikipia

Watu 15 wamelazwa katika hospitali mbali mbali kaunti ya Laikipia baada yao kuonyesha dalili za ugonjwa wa homa ya Nguruwe maarufu Swine Flu. Tayari mtoto mmoja anakisiwa kufariki kutokana na homa hiyo. Afisa wa kliniki kaunti hiyo Evelyn Obongo anasema wamewapokeza zaidi ya wagonjwa 60 na tayari 15 wameonyesha kuwa na dalili hizo. Obongo anasema watoto ndio walioathirika na homa hiyo. Idara ya afya kaunti hiyo aidha tahadhari imetolewa kwa wenyeji kujiepusha na homa hiyo ambayo husababisha joto jingi,maumivu ya viungo,kikohozi,mgonjwa kupiga chafia mara kwa mara na hata kukosa ari ya kula chakula.

Show More

Related Articles