HabariMilele FmSwahili

Shirika la haki Afrika lapendekeza kupunguzwa kwa idadi ya kaunti nchini hadi 10

Shirika la haki Afrika linapendekeza kupunguzwa hadi 10 idadi ya kaunti nchini. Shirika hilo pia linataka kuwepo wabunge 150 pekee. Afisa mkuu Hussein Khalid anasema hatua hiyo itakabili hali ya sasa ambapo taifa linakumbwa na changamoto mbali mbali ikiwemo baa la njaa na umaskini. Aidha anasema mishahara ya wabunge inapaswa kupunguzwa hadi shilingi laki mbili kwa wabunge na laki tatu kwa magavana.

Show More

Related Articles