HabariPilipili FmPilipili FM News

COTU Yaitaka Wizara Ya Leba Kutatua Mgomo Katika Hospitali Ya Kenyatta.

Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli ameitaka wizara ya leba kuingilia kati mgomo wa wafanyikazi unaondelea katika hospitali kuu ya Kenyatta ili huduma katika hospitali hiyo zirudi katika hali yake ya kawaida.

Atwoli ameeleza wasiwasi kuhusiana na masuala ya migomo huku akivitaka vyama husika kufuata miongozo iliyoko kabla ya kugoma.

Ameitaka wizara ya Leba kuteua msuluhishi kusaidia kutatua mgomo huo huku huduma za matibabu katika hospitali hiyo zikiendelea kuathirika.

Show More

Related Articles