HabariPilipili FmPilipili FM News

Bunge La Kwale Kujadili Mswada Kuhusu Kupigwa Marufuku Kwa Bidhaa Ya Miraa.

Bunge la kaunti ya Kwale leo linajadili hoja iliyowasilishwa na mbunge wa Kasemeni Anthony Yama ya kutaka ulaji wa miraa na mogokaa kupigwa marufuku katika kaunti hiyo.

Kulingana na Yama vijana wengi wa kaunti hiyo wameathiriwa na utumizi wa miraa na mogokaa jambo ambalo linawafanya kutojishughulisha na masuala yoyote ya ujenzi wa taifa na uchumi.

Kulingana naye baadhi ya wanaume wanashindwa kutekeleza majukumu yao ya kifamilia kufuatia kuathiriwa na utumizi huo.

Aidha amesema hawalengi kuua bishara ya miraa nchini akisema wasambazaji wa bidhaa hizo watafute soko sehemu nyingine na wala sio Kwale.

Spika wa bunge la kaunti hiyo Sammy Ruwa ataongoza kikao hicho.

 

Show More

Related Articles