People Daily

Serikali Yapiga Marufuku Vyakula Vya Nyama Kutoka Afrika Kusini

Serikali imepiga marufuku vyakula vya nyama vilivyotengenezwa na kampuni ya Afrika Kusini kwa jina Enterprise Food production na Rainbow Chicken.

Mkurugenzi wa afya ya umma dr Ken Ombacho anasema marufuku hiyo imechangiwa na mkurupuko wa maradhi ya Listeriosis Afrika Kusini.

Amezitaka kampuni zinazouza bidhaa hizo nchini kutekeleza marufuku hiyo mara moja ikiwemo kukoma kuuza bidhaa ambazo tayari zimesafirishwa.

Maradhi hayo ya Listerious yanasababisha maumivu ya viungo,joto jingi na hata kuendesha kwa baadhi ya watu.

Show More

Related Articles

Check Also

Close