HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Tani zaidi ya 75 za plastiki zimenaswa eneo la viwandani Nairobi

Licha ya marufuku ya matumizi na utengenezaji wa mifuko ya plastiki kuanza kutekelezwa mwaka uliopita,wakenya wamezidi kukaidi marufuku hiyo na kutumia na pia kutengeneza mifuko ya plastiki. Hii leo maafisa kutoka mamlaka ya kuhifadhi mazingira NEMA wamewanasa wafanyibiashara wawili wanaoaminika kuwa wakurugenzi wa kampuni moja inayohusika na utengenaji wa bidhaa hasa mifuko ya plastiki katika eneo la viwandani Nairobi. Msako wa leo ulitekelezwa pia katika masoko kadha kadhaa jijini huku wengi wa wafanyibiashara wakionekana kuzingatia marufuku hiyo.

Show More

Related Articles