HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili VideosVideos

Mgaagaa na Upwa : Julius Osoro japo ni kasisi anajipa riziki kwa kupiga viatu rangi

Ni msimu wa mvua, na japo mvua ni baraka kutoka kwa Maulana, kwa wengi hasa wanaoenda kazi afisini, huwa na kibarua cha ziada kwani viatu huchafuka na inabidi kuvipanguza kila wakati. Lakini japo ni kero, ni tabasamu zaidi kwa wanaopiga viatu rangi, huu ukiwa ni msimu wa kuvuna kwani wateja ni wengi. Mmoja wao ni Julius Osoro jamaa ambaye japo ni kasisi, amepata kufahamu kuwa kazi hii ya kupanguza viatu ina pesa za ziada, na kwa muda wa miaka 14 ameichangamkia. Basi huyu hapa Joab Mwaura na maelezo zaidi kwenye makala ya mgaagaa na upa wiki hii.

Show More

Related Articles