HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Imehimizwa Kusambaza Vifaa Vyakutosha Vya Matibabu.

Madaktari katika hospitali kuu ya Kenyatta Jijini Nairobi wameitaka serikali kusambaza vifaa vya kutosha kwenye hospitali hiyo ili kuwezesha utoaji wa huduma bora na kukomesha visa vya makosa ya matibabu.

Akiongea na wanahabari, daktari wa upasuaji kwenye hospitali hiyo David Kimani amesema vifaa wanavyotumia wakati wa huduma za upasuaji vimezeeka jambo ambalo linachangia kutokea changamoto kwa matatizo ambayo yanashuhudiwa.

Anasema wahudumu wa afya ni wachache pia jambo ambalo mara nyingi huchangia visa kama vya watoto kuibiwa kutokea kwenye hospitali hiyo.

Amesema wizara ya afya ilidai kukosa fedha za kuimarisha huduma za hospitali hiyo pamoja na vifaa, akisema licha ya serikali kutumia shilingi bilioni 34 za kuimarisha hospitali za humu nchini hospitali hiyo haikupata hata shilingi moja.

Kando na hayo anasema hospitali ya Kenyatta inakabiliwa na msongamano mkubwa wa wagonjwa licha ya kukosa vifaa muhimu.

Haya yanajiri huku huduma kwenye hospitali hiyo zikiendelea kuathirika.

Show More

Related Articles