HabariMilele FmSwahili

Wabunge kuandaa hoja ya kumbandua afisini waziri wa afya Sicily Kariuki

Wabunge wanaandaa hoja ya kumbandua afisini waziri wa afya Sicily Kariuki. Wakizungumza huko Mombasa wabunge hao wanadai Kariuki amekwenda kinyume na sheria kwa kumtuma likizo ya lazima mkuu wa hospitali ya Kenyatta Lily Korros. Wanadai Kariuki alipaswa kuendesha uchunguzi kuhusiana na upasuaji wa makosa kenyatta kabla ya kumtimua Koross aidha wametilia shaka utendakazi wa bi Kariuki wakidai ndiye aliyechangia kufeli kwa wizara ya vijana na jinsia miaka mitano iliopita.

Show More

Related Articles