HabariPilipili FmPilipili FM News

Jamaa Aomba Usaidizi Baada Ya Kupigwa Risasi Katika Sehemu Za Siri

Mwanaume  mmoja mwenye umri wa miaka 30 kutoka Kisauni Magogoni hapa Mombasa ameomba wahisani kujitokeza na kumsaidia kugharamikia matibabu yake baada ya kupigwa risasi kimakosa katika sehemu zake za siri na afisaa mmoja wa polisi

Jamaa huyo kwa jina Kisau Katana Muhambi anasema yuko katika hali ngumu ya kutafuta kazi na matibabu ya jeraha alilonalo, na changamoto kubwa anayopitia ni  kuwa anakosa msaada wa kuendelea na matibabu pamoja na pesa za kuhudumia familia yake.

Anasema kufuatia mkasa huo alipoteza nguvu zake za kiume na mkewe kumkimbia huku madeni ya kodi katika nyumba anayoishi yakimuweka katika hatari ya kufurushwa.

 

Show More

Related Articles