HabariMilele FmSwahili

Waziri Mucheru : Serikali ililazimika kuzima mawimbi ya runinga 3 nchini kutokana na changamoto za kiusalama

Serikali ililazimika kuzima mawimbi ya runinga tatu nchini kutokana na changamoto za kiusalama. Akihojiwa na kamati ya seneti ya habari wazairi wa habari na mawasiliano Joe Mucheru amesema hatua hiyo ilichukuliwa kufuatia mkutano wa baraza la kitaifa la usalama. Hata hivyo Mucheru amedinda kusema ni nani hasaa aliidhinisha hatua hiyo. Aidha ameskataa kujibu baadhi ya maswali ya maseneta kutokana na kile alikitaja kuwa sababu za kiusalama na kuwepo kwa kesai mahakamani.Waziri Mucheru amesisitiza kuwa licha ya hatua hiyo serikali itasalia kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari.

Show More

Related Articles