HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Kuja Ni Mikakati Yakuzuia Ufujaji Wa Pesa Za Umma Katika Kaunti.

Serikali kupitia wizara ya ugatuzi nchini inalenga kuja na mfumo utakaosaidia kutatua mizozo inayotokea baina ya serikali kuu na zile za kaunti, pamoja na makatibu katika idara mbali mbali za kaunti.

Akizungumza katika mkutano uliowajumuisha wazee wa mitaa na makamishna kutoka kaunti zote sita za Pwani,waziri wa ugatuzi nchini Eugine Wamalwa amesema fedha nyingi za umma zinafujwa kupitia mizozo hiyo ambayo imekuwa ikipelekwa mahakamani na kuchangia fedha nyingi za umma kutumika kiholela.

Wamalwa amesema ziko njia nyingi za kusuluhisha mizozo kando na kupeleka,kesi mahakamani zinazotumia miaka kutatuliwa.

Amesema endapo suala hili halitashughulikiwa basi huenda ndoto ya ugatuzi ikakosa kutimia.

 

 

Show More

Related Articles