HabariPilipili FmPilipili FM News

Himizo La Gavana Samboja Kwa Wakusanyaji Ushuru Taita Taveta.

Gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja amewataka maafisa wa serikali ya kaunti kuweka mikakati mwafaka katika ukusanyaji ushuru ili kufanikisha maendeleo ya kaunti baada ya kubainika kuwa mgao mkubwa wa fedha kutoka kwa serikali ya kitaifa hutumika kulipa mishahara.

Samboja ameunga mkono kilio cha magavana nchini kutaka serikali za ugatuzi kupewa fedha za kuwezesha utendakazi lakini akatoa tahadhari kwa vitengo husika kaunti yake kupiga jeki juhudi za kukusanya ushuru.

Kaunti ya Taita Taveta ni moja wapo ya kaunti kunashuhudiwa changamoto ya uvunaji haramu wa mchanga na ukataji miti kiholela kutoka kwa ranch ambapo hupoteza ushuru kutokana na shughuli hizo.

Kwa sasa serikali ya kaunti imetakiwa kubuni sera na miswaada itakayodhibiti biashara haramu kama makaa na uchimbaji mchanga ili kuwezesha maafisa wa utawala kuwachukulia hatua wahusika watakaopatikana.

Show More

Related Articles