HabariK24 TvMakalaSwahiliSwahili VideosVideos

Tandabelua la Machifu: Machifu wanashambuliwa Shinyalu-Kakamega kwa kutekeleza sheria

Kazi ya chifu, naibu wake na mzee wa kijiji huenziwa sana katika utawala wa mashinani ila sivyo katika eneo la shinyalu kaunti ya Kakamega. Viongozi wa utawala Kakamega huishi kwa hofu ya kushambuliwa na wenyeji wasiopendezwa na maamuzi yao ya kutatua mizozo. Mwenendo huu umeshuhudiwa tangu miaka ya sabini.  Wengi wao wamesalia na makovu kwa kuwashambulia kwa panga kila mara wanapojaribu kutekeleza sheria kijijini. Mwanahabari wetu Dennis Matara alizungumza na baadhi ya machifu ambao  wamekatwa mikono huko Shinyalu, Kakamega na kukuandalia makala ya Tandabelua la Machifu Shinyalu.

Show More

Related Articles