HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Mahakama kuu yasitisha kwa muda kesi dhidi ya Maina Wanjigi

Mahakama Kuu ya Milimani hapa Nairobi imesitisha kwa muda kuendelezwa kwa kesi ya uhalifu dhidi ya aliyekuwa wakati mmoja waziri kwenye serikali ya Rais mstaafu Daniel Arap Moi, babake mfanyibiashara mashuhuri, Jimmy Wanjigi, mzee Maina Wanjigi. Jaji Roselyne Aburili ameagiza kesi aliyokuwa amefunguliwa mzee Wanjigi kwenye mahakama ya Nyeri isitishwe ishara kuwa agizo la awali kwamba mzee Wanjigi ajiwasilishe mbele ya mahakama ya Nyeri kukana mashtaka yanayomkabili kwa sasa limesitishwa.

Show More

Related Articles