HabariPilipili FmPilipili FM News

Wavuvi Vanga Walalamikia Kunyanyaswa Na Askari Wa Tanzania.

Wavuvi kutoka eneo la Vanga kaunti ya Kwale wamelalamikia kunyanyaswa na askari jeshi kutoka nchi jirani ya Tanzania.

Wavuvi hao ambao huzalisha tani nne za samaki kila siku wameitaka serikali kuingilia kati jambo hilo na kuleta shuluhisho la kudumu kwani kwa sasa wanapitia hali ngumu na hawana uhuru wa kuvua samaki katika sehemu hio wakidai boti zao tatu zilikamatwa na askari jeshi wa Tanzania

Wakati huo huo wavuvi hao wameelekeza kilio cha kwa serikali kuhakikisha barabara ya eneo hilo inakarabatiwa ili kurahisisha usafirishaji wa samaki katika masoko ya mjini Mombasa.

 

Show More

Related Articles