HabariMilele FmSwahili

Duale ataka upinzani kukoma kukosoa kila hatua ya serikali

Kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale ametaka upinzani kukoma kuikosoa serikali kwa kila hatua inayochukua pasi na kutambua mazuri yanayofanywa kuwafaidi wakenya. Akihutubia kongamano la wabunge mjini Mombasa,Duale amesema upinzani unastahili kuchangia kuborehs maisha ya wakenya badala ya kukosoa kila ajenda ya serikali akisema hatua hiyo inaashiria ubinafsi.
Kwa upande wake,kiongozi wa wachachee John Mbadi ambaye amehutubia kongamano hilo amelalamikia kile anadai serikali kutoheshimu uhuru wa bunge na mahakama akisema hatua hiyo ni hatari kwa umoja wa taifa.

Show More

Related Articles