HabariPilipili FmPilipili FM News

Madaktari Wanaopokea Mafunzo Hospitali Ya Kenyatta Wamesitisha Huduma Zao

Madaktari wanaopokea mafunzo katika hospitali kuu ya Kenyatta wamesitisha huduma zao hadi pale serikali itakapowarudisha kazini afisaa mkuu mtendaji wa hospitali hiyo Lily Koros na mkurugenzi wa matibabu Benard Githae ambao walisimamishwa kazi wiki iliyopita baada ya hospitali hiyo kukumbwa na kashfa ya kumfanyia upasuaji mgonjwa kimakosa.

Katika taarifa iliyotolewa na muungano wa chama cha madaktari nchini KMPDU madaktari hao wametoa shinikizo la wakuu wao kurudishwa kazini bila masharti.

Naye mwenyekiti wa muungano huo Samuel Oroko amemtaka waziri wa afya nchini Sicily Kariuki kujiuzulu kwa kushindwa katika kazi yake kama waziri kutatua matatizo yanayoikumba hospitali kuu ya Kenyatta.

Tayari muungano huo umeunda kamati ya madaktari saba kuchunguza kisa hicho ili kuja na mwafaka wa mzozo huo.

Show More

Related Articles