HabariPilipili FmPilipili FM News

Jopo Kazi Litakalohakikisha Misitu Nchini inalindwa Laundwa.

 

Wizara ya mazingira nchini imezindua jopo kazi litakalohakikisha misitu ya humu nchini inalindwa dhidi ya shughuli za ukataji wa miti ya mbao.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa jopo hilo, waziri wa mazingira Keriako Tobiko amesema wameunda jopo hilo baada ya kugundua kuwa taifa hilo linakabiliwa na mgogoro mkubwa ikiwemo ukataji haramu wa mbao, mito kukauka miongoni mwa mengine.

Ametangaza kusimamishwa kwa shughuli zote za misitu katika kipindi cha siku 90 zijazo ili kutoa nafasi kwa jopo hilo kuendeleza kazi yake kabla ya kutoa mwelekeo zaidi.

 Wakati huo huo naibu rais William Ruto amesema serikali iliamua kuunda jopo hilo ili kukabiliana na changamoto ya uharibifu wa misitu.

Jopo kazi hilo lenye wanachama 17 linajumuisha wataalamu waliobobea katika masuala ya usimamizi haswa wa misitu na mazingira.

 

Show More

Related Articles