HabariMilele FmSwahili

Madaktari wanafunzi katika hosipitali ya kenyatta wasitisha huduma hospitalini humo

Madaktari wanafunzi katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta wamesitisha huduma hospitalini humo. Ni baada ya baadhi ya madaktari kuachishwa kazi kutokana na kisa cha kufanyiwa upasuaji wa ubongo mgonjwa mmoja kimakosa. Akitangaza hatua hiyo, katibu wa madaktari Ouma Oluga anasema madaktari hao zaidi ya 700 hawawezi kufanya kazi katika mazingira yasiyowatambua. Oluga ametaka pia madaktari walioachishwa kazi kurejeshwa mara moja akikosoa hatua ya waziri wa afya Siacly Kariuki ambaye aliwapa likizo ya lazima. Wakati huo KMPDU imeteuwa kamati ya watu 14 wakiwemo madakatri ambao pia wanafanya uchunguzi wao sambamba na ule unaofanywa na serikali kuhusu kilichojiri katika hospitali hiyo

Show More

Related Articles